Shitindi Poultry inapenda sana kutoa shukrani za dhati kwa wageni ambao ni wafugaji kutoka TABORA,IGUNGA.


Shitindi Poultry inapenda sana kutoa shukrani za dhati kwa wageni ambao ni wafugaji kutoka TABORA,IGUNGA.

 

 

ufugaji
mwalimu wa ufugaji mwenye uzoefu zaidi ya miaka 10 akitoa elimu

Tunayo furaha kubwa sana kwa kutembelewa na wageni kutoka tabora wilaya ya igunga, wageni hao walikua faraja sana kwetu kwa sababu tumejifunza mengi kutoka kwao na wao pia wamejifunza mengi sana kutoka kwetu pia..

wafugaji hao walikuja kama wawakilishi wa vijiji kumi vilivyopo huko igunga Tabora, wao walijifunza mengi sana kuhusiana na ufugaji na wakaahidi pia wataenda kuwapa wafugaji wenzao elimu bure kabisa kama jinsi wao walivoipata hapa SHITINDI POLTRY FARM.

 

shitindi
mwalimu wa ufugaji

zaidi tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kabisa kwa viongozi waliweza kufanikisha zoezi hili la kutoka tabora kuja mpaka dar es salaam kuja kujifunza, na pia bila kumsahau Daktari waliokua nao katika msafara huo ambae ni daktari kinara wa wilaya hiyo ya igunga katika ufugaji wa kuku, tulijifunza sana kwake na pia na yeye alikiri kua alijjifunza sana kwetu pia.

zaidi ya yote nawakaribisha tena na  tena kwa mara nyingine pale watakapopata nafasi zaidi ya kuja tena kujifunza tena, karibuni sana na sana..

Advertisements

TUNAUZA VIFARANGA WA KIENYEJI


Tunauza vifaranga wa kienyeji ambao ni bora zaidi kwa soko la mayai na nyama pia, Vifaranga wetu wako wa aina kadhaa..

  • Wapo wale wa MALAWI(weusi)
  • Pia wapo wale wekundu wa CANADA(RED FOWLS)
  • Pia wapo SASO wa Australia
  • Mwisho kabisa wapo na wa MOSHI ambao ni wazuri kwa mayaina nyama pia.

Kila kuku ana sifa yake na ana uzuri wake, na ndio maana tumewachanganya ili kwenye soko wawe wanaeleweka kwa maana ya mtu akitaka nyama atapata na mtu akipata mayai atapata pia..

karibu sana kwenye darasa la kila jumamosi ujifunze mambo mengi kuhusu ufugaji na unufaike, darasa ni bure kabisa, bila gharama zozote..

wasiliana nami kwa namba 0713 071 701

TUNATENGENEZA CHAKULA CHA KUKU BORA KABISA


Shitindi Poultry Farm tunatengeneza chakula  bora kabisa kwa kuku waliofikisha wiki tisa ambapo ni sawa na miezi miwili na wiki moja, tunafanya hivyo ili kupunguza gharama za ufugaji, kwa sababu ukifuga kuku wa kienyeji na ukawalisha chakula cha dukani kwa muda wa miezi minne mpaka watakapoanza kutaga ni hasara sana,  lakini SHITINDI POULTRY FARM tunakuletea suluhisho hilo kwa kukutengenezea chakula hicho kwa unafuu kabisa kuliko kile utakachonunua dukani…

Chakula tunachotengeneza ni kuanzia Finisher na Layers.

hii Finisher wanakula kuku wale walio na umri wa wiki tisa, na hicho Layers wanakula kuku walioanza kutaga baada ya kula finisher mpaka pale watakapoanza kutaga.

Karibu sana ujipatie chakula bora na kwa bei nafuu kabisa kama ya bure.

tunapatikana kimara Temboni Mrogoro road….. pia tunakua na semina kila jumamosi kuanzia saa tano asubuhi kamili tukijifunza habari za ufugaji wa kuku wa kienyeji.

semina ni bure kabisa, karibu sana ujifunze.

mawasiliano yetu ni 0713071701

CAGES ZINAPATIKANA KWA WINGI


Jipatie Cage yako sasa, Cage ya kisasa kabisa iliyo ya kudumu na isiyoshika kutu.

Cage zetu ni imara sana na zina uwezo wa kubeba kuku wengi na bila kuharibika,

cage zetu zina

  1. Automatic drinkers,(nipples zisizomwaga maji chini kama cage nyingine).
  2. Ni ngumu na imara ambazo hazielemewi na uzito wa kuku tofauti na nyingine.

Tunakusafirishia mpaka mahali ulipo ukiwa ndani ya dar es salaam na kukufungia bure kabisa baada ya kununua.

cage hizi zinapatikana SHITINDI POULTRY FARM TU..

KARIBU SANA.

mawasiliano yetu ni 0713071701

USHAURI JUU YA SOKO LA MAYAI NA KUKU WA KIENYEJI


Ufugaji wa kuku ni ujasiriamali ambao watu wengi hufanya kama kitu cha ziada sana.

Lakini wasitambue kua ni Ujasiriamali ambao unaweza ukaingiza kipato cha kuendesha maisha yako na ukaishi maisha mazuri bila shida… Mimi ni mfugaji wa muda mrefu sdana na nilianza kama masihara bila kupanga kua ndio kazi ambayo itakua inaniingizia kipato kwa wingi katika maisha yangu ya kila siku…

Nikizungumzia ujasiriamali nalenga hasa vijana maana ndio nguvukazi katika jamii, na ni mara nyingi hasa vijana wamekua wakiidharau kazi hii ama ujasiriamali huu wa ufugaji wa kuku.

Napenda sana kuwashauri vijana wenzangu wajiingize katika ujasiriamali huu bila kujali kua amesoma kiasi gani ili aweze kuingiza hela kwa wingi na aweze kukidhi maish aya kila siku kama mtanzania mwinigne bila shida yeyote..

ufugaji sio mgumu, ila tu watu ndio wanaufanya uonekane mni mgumu… hasa wa kuku wa kienyeji ambao wanaweza kukuingizia kipato mara mbili kwa maana ya MAYAI na KUKU wenyewe kwa uuzaji wa nyama…

Watu wengi huogopa swala la soko, wala sio gumu, kwa sababu kabla ya kuanza kufuga inabidi kutafuta soko kwanza na sio tu kuanza kufuga bila  kujua ni wapi utauza kuku wako ma mayai utakayoyazalisha.

Fanya utafiti kwanza kabla ya kuanza kufuga, tafuta masoko kwanza , JUA ni wapi na wapi nitauza mayai au kuku nitakaowazalisha.

1:Pita mahotelini wanapouza vyakula vya kula kila siku.

2:Pita mashuleni ulizia soko pia.

3:Pita madukani pia ulizia kuhusu masoko ya mayai na kuku(kwa nyama)

BAADA YA HIZO HATU HAPO NDIO UTAWEZA KUJU AWAPI UNANZIA NA WAPI UTAISHIA NA KAZI ZAKO ZITAENDAJE PAMOJA NA UZALISHAJI BORA WA KUKU NA MAYAI.

KARIBU SANA KWA USHAURI ZAIDI

0713 071 701

Tunauza incubator za aina zote(mashine za kutotoleshea)


SHITINDI POUTRY FARM tunauza mashine za kutotoleshea(incubator) za aina zote na zenye ubora.

Mashine zetu zina ubora wa kiwango cha hali ya juu na zinaweza kustahimili hali ya hewa ya aina yeyote.

Vile vile mashine zetu ni full automatic, yaani zinafanya kazi kwa kujitegemea.

karibu sana ujionee mashine zenye ubora nan zenye viwango tofauti kutegemea na matumizi yako.

kwa mawasiliano piga simu namba 0713071701

karibu kwenye Semina ya kuhusu ufugaji wa kuku wa kienyeji kila Jumamosi.


SHITINDI POUTRY FARM inakuletea semina za kila jumamosi ambazo zitakua zinafanyika Kimara Temboni dar es salaa..

unakaribishwa kuja kujifunza bure kabisa bila malopo ya aina yeyote ni muda wako tu.

 

Kwenye semina zetu utajifunza mambo muhimu yafuatayo.

1:Chanjo zote kuanzia kifaranga hadi akianza kutaga,

2:Namna ya kuwalisha kuku wako vizuri kwa afya na wakakua kwa haraka.

3:Namna ya usafi.

4:Jinsi ya kuchanganya chakula cha kuku kupunguza gharamam za ulishaji.

na mambo mengine mengi,

 

Na pia katika semina hizo utaruhusiwa kuulizxa kitu chochote kuhusiana na ufugaji wa kuku wa kienyeji.

ukihitaji maelezo ya kufika wasiliana nasi kwa namba zifuatazo 0713071701

Create a free website or blog at WordPress.com.

Up ↑

%d bloggers like this: